Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye Bungeni leo amesema hadi kufikia Aprili 30, 2022 jumla ya anuani za makazi 12,171,320 zimekusanywa na kuingizwa kwenye programu tumizi.
“Idadi ya anuani zilizokusanywa ni 104.3% ya lengo la jumla ya anuani 11,676,891 zilizopangwa kukusanywa katika Mikoa yote nchini, matumizi ya programu tumizi yamewezesha kubaini maeneo mengineyo yaliyokuwa hayajabainishwa na Mamlaka za Serikali za Mitaa”- Waziri Nape
“Kufuatia malengo ya Serikali ya kukamilisha anuani za makazi kabla ya Sensa ya Watu na Makazi itakayofanyika Mwezi Agosti, 2022, Rais Samia alielekeza mfumo huo kutekelezwa kwa operesheni, aliyoipa jina la “Operesheni Anuani za Makazi”- Waziri Nape
“Programu tumizi imetumika katika kukusanya taarifa za barabara/ mitaa/ njia, makazi na wakazi sambamba na kumuongoza Mtu kutoka anuani ya makazi moja kwenda anuani ya makazi nyingine”- Waziri Nape
“Semina ya kuwajengea uelewa kuhusu mfumo wa anuani za makazi imetolewa kwa Viongozi 483 ambao ni Wakuu wa Mikoa, Katibu Tawala wa Mikoa, Wenyeviti na Wakurugenzi wa Halmashauri, Wataalamu 616 wa Mikoa na Halmashauri wamejengewa uwezo kuhusu namna bora ya kutekeleza mfumo huo ili wasimamie ipasavyo katika maeneo yao”- Waziri Nape