Licha ya Rais wa Jamhuri ya muungano Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kuzindua Royal tour lakini pia ameendelea kuboresha miundombinu katika vivutio vya utalii katika maeneo mbalimbali nchini.
Hapa ni pori la akiba Wami Mbiki ambalo lipo chini ya TAWA Rais Samia kupitia fedha za UVICO 19 ametoa zaidi ya Bilioni 2.3 kwa ajili ya kujenga miundombinu mbalimbali ikiwemo Barabara na nyumba za watalii .
Emanuel Lalashe Ni kamanda wa pori hilo la akiba Wami Mbiki anasema fedha hizo zitasaidia Katika kuboresha shughuli za utalii katika eneo hilo .
Pori Hilo awali lilikua chini ya wananchi jumuia ya uhifadhi Wanyama pori kabla ya mwaka 2012 kushindwa kujiendesha ambapo mwaka 2021 pori hilo lilipandishwa hadhi na kuwa pori la akiba na kuwa chini ya TAWA
Kwa upande wake afisa habari TAWA Beatus Maganja amesema mamlaka hiyo inakila sababu ya kumshukuru Rais Samia kwani ameendelea kutoa fedha katika maeneo mbalimbali yaliiyopo chini ya Mamlaka hiyo
Maganja anasema kwa upande wa serikali imejitahidi kuboresha miundombinu hivyo watajitahidi fedha hizo zitumike Kama zilivyokusudiwa.
Naye afisa uhusiano TAWA Joyce Nduguru ametoa wito kwa wananachi wanaoshi karibu na pori Hilo kuwa mfano bora kwa kutembelea ili kujionea vivutio vilivyopa
Joyce anasema suala la kutangaza utalii sio jukumu la mtu mmoja hivyo Kila Mwananchi anapswa kuwa mfano badala ya kuachia watalii kutoka nje ya Nchi pekee.
Pori hilo la Wami Mbiki linapatikana Mkoa wa Morogoro Wilaya Morogoro,Mvomero na Bagamoyo kwa upande wa mkoa Pwani na linaukubwa kilometa za mraba 2500
BANDARI YA TANGA KUKUSANYA TRIONI 1 KWA MARA YA KWANZA “SYSTEM INASUMBUA TUSAFIRISHE MKONGE”- MBUNGE