Wabunge na viongozi mbalimbali wa Serikaliwanatarajiwa kuelimishwa kuhusu Mamlaka yaUdhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) nashughuli inazozitekeleza kwenye Maonesho yaMajukumu ya Wizara ya Nishati na taasisi zake.
Maonesho hayo yaliyoanza rasmi leo, Mei 23, 2022 katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma yanaongozwana kaulimbiu isemayo ‘Nishati kwa MaendeleoEndelevu’ na yatafikia tamati Mei 26, 2022.
Kwa mujibu wa Waziri wa Nishati Mhe. January Makamba, maonesho hayo yanalenga kujibu maswaliya wabunge juu ya masuala mbalimbali ya sekta yanishati na kutatua changamoto mbalimbalizinazohusiana na sekta.
Wataalamu wa PURA wamejipanga kuongeza uelewakwa wabunge hao kwa maeneo mbalimbali ikiwemo yamradi wa kubadili gesi asilia kuwa kimiminika (LNG), ushiriki wa wazawa kwenye miradi mbalimbali yasekta ndogo ya mafuta na gesi asilia pamoja na fursambalimbali zinazopatikana kwenye utekelezaji wamiradi ya mkondo wa juu wa petroli.
Mjiolojia Ebeneza Mollel ameeleza kuwa maoneshohaya ni jukwaa muhimu kwa PURA kuwafikiawananchi kupitia viongozi wao kwa kuwaongezeauelewa na namna bora ya kutumia fursa zinazopatikanakatika utekelezwaji wa miradi mbalimbali ya mafuta nagesi asilia.
“Viongozi hawa ni kundi muhimu kufahamu fursa hizikwani wanaweza kufikia wananchi kwa urahisi zaidiikiwa ni pamoja na kuwasaidia na kuwajengea uwezowa jinsi ya kuchangamkia fursa hizi,” alieleza.
Naye Mjiolojia Wangese Matiko amebainisha kuwawabunge watakaotembelea banda la PURA pia watapata fursa ya kujifunza masuala ya kiufundi kamaya mnyororo wa thamani wa mafuta na gesi asilia, shughuli za utafutaji na uzalishaji zinazoendelea nchinina mengineyo.