Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi leo Mei 31, 2022 ameweka wazi kuwa Vita ya Ukraine imeathiri kwenye Bidhaa za Vyakula na Mafuta.
Rais wa Zanzibar amebainisha kuwa Serikali ya Zanzibar inaendelea Kufidia kwenye Bidhaa za Mafuta na Vyakula kwa Kupunguza Ushuru ili kuzuia Mfumko wa Bei.
‘Kama Mnavyo fahamu Ukraine ni wazalishaji wakubwa wa Bidha Kadha za Chakula ikiwemo Ngano, na Kwa sababu ya Vita Vile imesababisha Badhi ya Nchi kuzuia kusafirisha Nje ya Nchi zao bidhaa kadhaa kwa sababu ya matumizi yao’- Rais Mwinyi
‘Hio imeathiri sana hususani Biashara za Hapa Zanzibar Serikali imefidia kwa kiwango Kikubwa sana Bei ya Mafuta ya Dizeli ,Petroli na Mafuta ya Taa ,bei inayouziwa Bidhaa hizo hapa Zanzibar sio bei halisi ni bei iliofidiwa sana na Serikali’- Rais Mwinyi
“Kwa upande Mwingine tumepunguza ushuru Katika bidhaa za Vyakula Lengo ni kujitahidi Kuzuia Mfumuko mkubwa wa bidhaa Ambao kama tungeachia huenda kwa Hali ya Dunia ilivyo Sasa hivi izo bei za bidhaa zingekuwa bei juu mnoo”- Rais Dkt Mwinyi