Shafih Selemani (12) ni Mwanafunzi wa darasa la tano Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko Dar es salaam akiwa ni mwenye ulemavu wa macho lakini mwemye vipaji vingi ikiwemo kipaji cha kutangaza mpira “Darasani masomo pia nipo vizuri sing’oki 10 bora, mtihani wa Taifa darasa la nne nilipata ufaulu wa A”
“Mechi tatu tu zinanitosha kuvijua vikosi vyote, navijua vikosi vya Simba, Yanga, Azam na sasa nataka kuvijua na vingine kama Namungo, Geita n.k , Mama yangu kipato chake sio cha juu, natamani nikue hata kesho nimsaidie Mama yangu, sisi tumepewa tu nyumba ya hifadhi ya muda, Mama yangu hata akipatiwa msaada wa chumba kimoja tu cha kuishi kitatusogeza”
“Mwenyewe natamani nisaidiwe vitu vya kufanyia mazoezi kama ngoma, voice recorder kwa ajili ya kujirekodia mwenyewe wakati nikitangaza, radio, sare za Shule, daftari na vitu vingine”