Waziri wa Nishati January Makamba amewataka Watanzania kupuuza taarifa zinazosambaa toka jana kwamba Serikali imepandisha bei ya umeme nchini Tanzania.
Akijibu swali la Mbunge wa Nyasa Stella Manyanya, Waziri January Makamba amesema “si kweli kabisa kwamba bei ya umeme imepanda, Serikali inasikitishwa na wale wanaoeneza maneno hayo na uvumi huo kwenye mitandao na tumeomba Mamlaka husika zichukue hatua kwa udanganyifu na upotofu huo unaofanywa”
“Mchakato wa kupandisha bei ya umeme ni mrefu, unahusisha maombi ya TANESCO kwa EWURA na unahusisha public hearing kwamba Wananchi lazima wahusishwe na washirikishwe katika kutoa maoni yao pale bei ya umeme inapopandishwa, ni mchakato mrefu ambao hauwezi kufanyika kwa siri kwahiyo hizi taarifa kwamba Serikali imepandisha bei ya umeme sio kweli na naomba zipuuzwe” ——— asema Waziri January Makamba