Rais wa club ya Al Ahly ya Misri Mahmoud El-Khatib ameweka wazi mtazamo wake na mapendekezo yake kwenda kwa Shirikisho la soka Afrika CAF kufuatia kupoteza kwa timu yake 2-0 katika mchezo wa fainali dhidi ya Wydad Casablanca ya Morocco.
Mahmoud anaamini kuwa sasa ni wakati sahihi kwa CAF kurudisha mfumo wa zamani kwa kuchezwa kwa fainali mbili za nyumbani na ugenini katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho Afrika kwa sababu mfumo wa mchezo mmoja umefeli.
Miongoni mwa sababu zinazotajwa Mahmoud zilizosababisha aseme mfumo huo umefeli ni kutokana na Afrika miundombinu ya kusafiri sio sawa na Ulaya na gharama yake iko juu kingine Afrika hawatumii noti moja kama Ulaya, matatizo ya mashabiki kupata visa.
Bibo ameyasema hayo baada ya fainali mbili za Ligi ya Mabingwa kuchezwa Morocco lakini pia mashabiki wengi wa Al Ahly walikwama kuingia Morocco sababu za masuala ya visa na usafiri pia.