MSTAHIKI Meya wa Manispaa ya Morogoro Mhe. Pascal Kihanga, amewataka Viongozi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Morogoro kufanya kazi kwa kuzingatia uadilifu ili vyama hivyo viweze kufikia malengo waliyojiwekea.
kihanga ametoas wito huo juni 21 mwaka huu wakati wa ufunguzi wa Jukwaa la Maendeleo ya Ushirika Mkoa wa Morogoro ambapo amesema wapo baadhi ya watumishi wa vyama hivyo sio waadilifu jambo ambalo linarudisha nyuma jitihada za serikali kuwakomboa wakulima kupitia ushirika.
Akizungumza katika Jukwa hilo, Mhe. Kihanga, amesema kutofanya kazi kwa kuzingatia uadilifu kuna pelekea ubadhilifu wa fedha pamoja na migogoro ndani ya ushirika.
“Lazima mfanye kazi kwa uadilifu , msiruhusu migogoro,mkiwa na migogoro hata wale wanaotaka kutoa misaada hawatawaletea tena, simamieni miiko ya Uongozi ili Wanachama wenu waweze kunufaika na Ushirika huu” Amesema Kihanga.
Aidha, Kihanga, amewataka Viongozi kufanya kazi kwa kusimamia sheria na kanuni badala ya kufanya kazi kwa mazoea jambo ambalo halitawafikisha mbali na kutofika mafanikio au malengo waliojiwekea.
Hata hivyo, amewataka Viongozi wa Vyama vya Ushirika kuhakikisha katika Mikutano yao agenda kubwa iwe uadilifu ili kujenga uwaminifu kwa wanachama wao.
Kuhusu changamoto ya vyama vya mazao, amezitaka Taasisi za kifedha kuvitembelea vyama hivyo na kuweza kutatua changamoto zao.
Naye Mwenyekiti wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Morogoro, Idd Rajabu, amesema lengo la Mkutano huwa wa Jukwaa la Vyama vya Ushirika ni kuwakutanisha wana Ushirika na wadau wake kwa ajili ya kujengeana uwezo na uzoefu ili kujenga Ushirika Imara na wenye nguvu.