Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro June 14, 2022 amefanya ziara katika eneo la Loliondo, Ngorongoro kwa ajili ya kujionea zoezi linaloendelea la uwekaji alama za mipaka, ambapo ameeleza kuridhishwa kwake na kasi iliyopo.
IGP Sirro ambaye alifuatana na Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongella, amewataka washiriki wa zoezi hilo kujituma ili kazi ya uwekaji alama za mipaka katika eneo hilo iishe kwa wakati.