Wananchi wa Kigamboni wameanza kufurahia huduma ya haraka ya uvushaji wa abiria iliyoanza kutolewa jana na Vivuko vya Azam Marine wakati huu ambapo Vivuko vilivyokuwa vikitumika kwenye eneo hilo vikifanyiwa matengenezo.
Baadhi ya Wananchi walioongea na AyoTV wameelezea kufurahishwa na uharaka wa vivuko hivi ambavyo vinachukua chini ya dakika 10 kutoka Magogoni hadi Kigamboni tofauti na ilivyokuwa kwa Vivuko ambavyo vimekuwa vikitumika kwa muda wote ambavyo vimekua vikichukua muda mrefu zaidi.
Jana Serikali kupitia Wakala wa Ufundi na Umeme (TAMESA) ilitangaza kufikia makubaliano na Kampuni ya Azam Marine kutoa huduma ya kuvusha Abiria kati ya Magogoni na Kigamboni ili Wananchi wapate huduma ya uhakika wakati huu ambao Wakala unaendelea kufanyia matengenezo vivuko vyake ambapo taarifa hiyo ilisisitiza Wananchi kutotumia mitumbwi kwenye kuvuka eneo hilo kwani ni hatari kwa usalama wao