Waziri wa Fedha na Mipango Dr. Mwigulu Nchemba akiwasilisha Bungeni mapendekezo ya Serikali kuhusu makadirio na mapato na matumizi kwa mwaka 2022/2023 amesema moja ya mkakati uliopo ni kubana matumizi yasiyo ya lazima kwenye ununuzi na matumizi ya Magari kwani ni moja ya vinavyoisababishia Serikali kutumia pesa nyingi zaidi.
Dr. Mwigulu amesema “Hatua za muda mfupi zitakazochukuliwa ni pamoja na kupunguza safari za ndani na nje, kukata fedha za ununuzi usio wa lazima, kupunguza ukubwa wa uwakilishi kwenye mikutano ya ndani na nje, tutapimiana mafuta ya magari ya Serikali kila mwezi kufuatana na shughuli za lazima”