Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ameitaka bodi mpya ya Taasisi ya Saratani ya Ocean Road kufanya tafiti za Dawa za Saratani ili kujibu maswali ya wananchi ikiwa ni pamoja na ukweli kuhusu madai ya Tunda la Stafeli kutibu saratani.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati akizindua bodi mpya ya Taasisi hiyo pia ameitaka kuweka Mpango mkakati wa miaka 15 wa kufungua vituo vya saratani katika hospitali za Rufaa.
“Tunataka utafiti kuhusu Dawa za saratani tunasikia stafeli inatibu saratani tunataka wataalamu watafiti watuambie kama ni kweli tujue ni majani, au maganda tujue hivyo wataalamu mnisaidie kutafiti hizo dawa mje na ushahidi wa kisayansi kama zinatibu au hazitibu,”amesisitiza.