Rais wa Urusi, Vladimir Putin amewajibu Viongozi wa Nchi za Magharibi ambao walikejeli picha zake za kifua wazi wiki hii kwa kusema Watu watachukia wakiwaona Viongozi hao wa Magharibi wakivua nguo zao kama yeye kwakuwa hawana muonekano wa kuvutia kama wake.
Kauli ya Putin inakuja baada baada ya Viongozi katika mkutano wa G7 kukejeli tabia ya Puti kujiweka bila shati kwenye picha, Putin amewaambia Viongozi hao kuwa wanapaswa kuacha kunywa pombe na wafanye mazoezi zaidi ili wawe na muonekano utakaowapa ujasiri wa kukaa kifua wazi.
Putin amesema “Ili kila kitu kiwe sawa lazima uache kutumia pombe vibaya na maovu mengine, kufanya mazoezi, kucheza michezo, hao Viongozi walionikejeli (akiwemo Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson), nawafahamu wote binafsi na hatuko kwenye kipindi bora cha mahusiano yetu, hilo linaeleweka”
Putin amesema “Nawashauri ukiwa Kiongozi ni lazima ujitunze, na kama wanapata muda wa kunizungumzia nawapongeza kwa hilo”