Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania IGP Simon Sirro amefanikisha ndoto yake ya kujenga Kanisa ndani ya Kijiji alichozaliwa cha Muliaza Wilayani Butiama ambapo amefanikisha ndoto hii kwa kushirikiana na Watu wengine waliomchangia fedha na vifaa vya ujenzi.
IGP Sirro amewataka Watu kuendelea kukumbuka nyumbani kwao wanakotoka na kusaidia jitahada mbalimbali za kuleta maendeleo na kusema anaamini kujenga kwake kanisa kutasaidia kupunguza uhalifu zaidi kwani wengi watakua wanalelewa kiroho na Viongozi wa dini.
Ufunguzi wa kanisa hilo la kigango cha Mulianza ulifunguliwa na Muhasham Askofu Simon Masondole Askofu mkuu wa Jimbo la Bunda na kumpongeza IGP Sirro kwa hatua aliyoichukua ya kujenga nyumba hiyo ya ibada.