Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi, Shaka Hamdu Shaka ametahadharisha agenda ya katiba mpya kubebwa na wanasiasa akisisitiza CCM inataka mchakato huo ushirikishe wananchi na kwamba hakuna dharura katika kuandaa katiba mpya.
Akizungumza wakati wa ziara yake katika Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) leo Julai 4 jijini Dar es Salaam, Shaka amesema “Katiba Mpya sio hoja ngeni kwa CCM. Hatukatai kuwa na mabadiliko, hakuna udharura wa kufikia mchakato huo tunachotaka wananchi kwanza washirikishwe na wao waseme wanataka katiba ya aina gani.”
Shaka amesema agenda ya katiba mpya haipaswi kuwa ya wanasiasa. “Tumefanya mabadiliko ya katiba ya sasa mara 14. CCM ni chama kiongozi, lazima itoe mwongozo kuhakikisha maslahi mapana ya taifa,” ameongeza.