Rais Samia Suluhu Hassan ameondoka nchini kuelekea Dakar, Senegal, kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi za Afrika wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kimataifa (IDA Summit for Africa).
Katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere mkoani Dar es Salaam, Rais Samia ameagwa na Viongozi mbalimbali akiwemo Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango.