Tume ya Maendeleo ya Ushirika ya Taifa kuviunganisha vyama vya ushirika ili kusaidia wafanyabiashara kuweza kupata mikopo ya kuinua biashara zao katika kupata masoko.
Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo Mrajis Msaidizi, wa Mkoa wa Dar es Salaam, Abdilah Mutabaz, jijini Dar es Salaam, kwenye maonyesho ya 46 ya Kimataifa, Sabasaba, amesema lengo la kuwa kwenye maonyesho ni kuviunganisha vyama vya shirika kupata fursa mbalimbali.
“Tunaonyesha kijiji cha ushirika ili kusaidia kupata wateja na wadau kupata fursa kuongea na vyama vya ushirika, kujiunga na vyama vya ushirika vinayojihusisha na kilimo cha Korosho, tumbaku pamba na alizeti.”
“Ushirika kuna wanaojihughulisha na mikopo ambao wanakopesha wafanyabiashara mbalimbali tunaamasisha watanzania kujionga na vyama cha ushirika iliwaweze kupata mikopo kusaidia kuinua biashara zao.” amesema Mutabaz
Kwa upande wake Ibrahim Kadudu-AR-PC maonyesho ya 46 ya Kimataifa, amesema kijiji cha ushirika na vyama vya ushirika ambavyo vimesajiri ni matokeo ya tume ya ushirika.
“Vyama vikikutana vinasaidiana vyenyewe kwa vyenyewe na baadae wanatafuta masoko ya nje ili kupeleka bidhaa zao mbali zaidi.”
“Chama cha ushirika kutoka Uganda wapo watanzania waje kuona bidhaa na kwanini tunakuwa na Ushirika wa kilimo fedha na madini katika kutafuta masoko na kuonyesha fursa mbalimbali.Wanakutana na kuunganisha mazao wanauza kwa ushirika na kuweza kuuza bidhaa nyingi kwa wakati mmoja.” amesema Kadudu