Aliyekuwa Mkurugenzi wa mradi wa Usafirishaji wa Mabasi yaendayo Haraka Dar es Salaam, (Udart) Robert Kisena(47) na wenzake wawili, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka 25 ikiwemo wizi, kutakatisha fedha, kuisabaishia Serikali hasara ya Sh. Bilioni 4.4 pamoja na kuongoza genge la uhalifu.
Washtakiwa hao wamesomewa mashtaka yao leo na Wakili wa Serikali, Timotheo Mmari akisaidiana na Aboud Yusuph, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi.
Mbali na Kisena washtakiwa wengine katika kesi hiyo ya Uhujumu uchumi namba 40 ya mwaka 2022 ni Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Simon Group Ltd, Charles Newe(48) na mfanyabiashara Kulwa Kisena(34).
Kesi hiyo imeahirishwa hadi July 18, 2022 huku upelelezi ukiwa umekamilika, ambapo unafanyika mchakato wa kesi hiyo kupelekwa Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumiy “Mahakama ya Mafisadi”.