Club ya Arsenal imecheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Nurnberg ya Ujerumani ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya msimu wa mpya wa Ligi Kuu England 2022/2023.
Katika mchezo huo uliyomalizika kwa Arsenal kushinda 5-3 kivutio kikubwa ilikuwa ni staa wao mpya Gabriel Jesus Raia wa Brazil aliyejiunga nao akitokea Man City.
Jesus huo ulikuwa mchezo wake wa kwanza na ilimchukua sekunde 90 tu kuifungia Arsenal goli lake la kwanza Kocha wa Arsenal akimuungiza dakika ya 46 kuchukua nafasi ya Pepe na dakika ya 47 akafunga goli Arsenal wakati huo ikiwa nyuma 2-0.
Gabriel Jesus alikuwa na bahati na kufanikiwa kupachika magoli mawili jumla katika ushindi wa Arsenal wa 5-3 dhidi ya Nurnberg Jesus akifunga goli lake la pili dakika ya 75 huku likiwa la tano kwa Arsenal.
Magoli mengine ya Arsenal yalifungwa na Mohamed Elneny dakika ya 54 na mawili mengine Nurnberg wakijifunga kupitia kwa wachezaji Schindler dakika ya 57 na Handwerker dakika ya 63.