Katika Hali isiyo ya kawaida baadhi ya vyoo katika wodi ya wanawake hospital ya Wilaya Ulanga vimefungwa kutokana na kukosekana kwa huduma ya maji kwa mda mrefu jambo lililopelekea usafi wa nguo,vyoo, na wodi kufanyika kwa shida.
Hayo yamemwa na baadhi ya wananchi na wakazi wa mji wa Mahenge baada ya mbunge wa Jimbo la Ulanga Salim Hasham kutembelea katika hospitali hiyo ili kusikiliza changamoto zilizopo katika eneo.