Wizara ya Afya kupitia kwa Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu imetangaza uwepo wa mlipuko mpya wa ugonjwa wa Homa ya Mgunda unaosababisha wananchi kutoka damu puani na kuishiwa nguvu na hata kufariki.
Ugonjwa huo wa Homa ya Mgunda unasababishwa na wanyama kama vile panya, bweha na swala.
Ugonjwa huu huambukizwa hupitia mkojo wa wanyama kwenye vyanzo vya maji ambapo tayari dawa imepatikana sanjari na namna ya kujikinga.
Hadi sasa wananchi 20 wameugua ugonjwa huo wilayani Ruangwa mkoani Lindi na wengine watatu kufariki, huku wawili wakiwa kwenye uangalizi maalumu.