Kampuni ya Ndege ya Air Tanzania leo imeanza safari ya kwenda Guangzhou nchini China ambapo ni safari ya moja kwa moja kutokea Tanzania.
Nauli kwa daraja la kawaida ni USD 4.800 ( Sawa na 11,186,302.05), huku daraja la Biashara ikiwa ni USD 6,850 sawa 15,963,785.22). ambapo hizo ni nauli za kwenda tu.
Katika taarifa yake ya awali, ATCL imebainisha ya kuwa tiketi zote zitauzwa katika Ofisi za Air Tanzania makao makuu.Hivyo ATCL haitahusika na tiketi itakayonunuliwa kwa bei tofauti.
Pia imesema inapitia upya takwa la karantini la siku 5 na gharama zake kwa wasafiri waendao Guangzhou ili kuhakikisha kuwa hakuna msafiri mwenye maambukizi ya UVIKO-19 ambaye atasafiri na ATCL.