Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Camilius Wambura amewaomba Wananchi hususani Wakazi wa Arusha kushirikiana na Polisi kwa kutoa taarifa za Wahalifu na wote wenye kuchafua taswira ya nchi na Arusha kwa ujumla.
IGP Wambura amesema Jeshi la Polisi limejipanga kuhakikisha amani na utulivu unakuwa wa kutosha.
Wambura ameyasema hayo leo July 21,2022 Jijini Arusha wakati akitoa taarifa juu ya ujio wa Marais wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambao watafanya mkutano Arusha July 22,2022.