Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Dr. Mohamed Nyembea amethibitisha kuongezeka kwa kifo cha Mwanafunzi mmoja wa Shule ya King David ambaye alikuwa miongoni mwa majeruhi Watano waliokuwa katika hali mbaya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Ligula.
Kifo chake kinafanya idadi ya vifo kufikia Watu 11 huku wawili kati yao wakiwa ni Dereva na Msaidizi ambapo miili ya Wanafunzi hao inatarajiwa kuagwa leo saa tisa alasiri katika Hospitali ya Rufaa ya Ligula.