Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana amemshauri Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Camilius Wambura kufanya tathmini kuhusu utendaji wa Jeshi la Polisi Kitengo cha kikosi cha Usalama barabarani.
Kinana amesema malalamiko dhidi ya Polisi hao yamekithiri kwa Wananchi na wamiliki wa Vyombo vya Usafiri vya Moto hususani Magari na Pikipiki.