Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema toka July 18,2022 hadi asubuhi ya leo hakuna Mgonjwa mpya aliyeonesha dalili za kuwa na ugonjwa wa Homa ya Mgunda ambapo amewasisitiza Wananchi kutokuwa na hofu kwakuwa ugonjwa huo umedhibitiwa na pia Serikali ina uwezo wa kuendelea kuchunguza, kutibu na imeweka mikakati ya kuudhibiti ugonjwa huu nchini.
Akiongea na Waandishi wa Habari Dar es salaam leo, Ummy amesema “July 18 nilikuwa Ruangwa Mkoani Lindi na nilitoa taarifa juu ya uwepo wa Homa ya Mgunda kwahiyo tumethibitisha rasmi ugonjwa wa Mgunda upo Tanzania na sio mara ya kwanza kugundilika nchini mwaka 2014 ulibainika Kigoma”