Kwa miaka sasa wateja wa KFC chini China wamekuwa wakishangaa kwanini kampuni hiyo imekuwa haiuzi miguu ya kuku, chakula ambacho kinapendwa na wengi nchini humo.
Hivi sasa, Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Yum China Joey Wat ameliambia shirika la habari la CNN kuwa
“naomba kuripoti kuwa kwa mwaka huu 2022, hatimaye tunauza miquu ya kuku”
Sababu kubwa ya mabadiliko hayo ni mlipuko wa bei.
Bw.Wat amesema kuwa “tunajaribu kubana matumizi kwa kutumia kila kitu kinachoweza kuliwa”
“Athari za janga la corona na kupanda kwa bei ya mafuta na chakula kwa ujumla zimeongeza sana gharama za biashara.
Kampuni ya Yum China yenye makazi yake Shanghai ndiyo inayomiliki KFC, Pizza Hut a Taco Bell chini China.