Siku moja baada ya Serikali kutangaza tarehe 23 Agosti kuwa siku ya mapumziko kitaifa kwaajili ya Sensa ya watu na makazi mbunge wa jimbo la Ushetu Emmanuel Cherehani amewaomba wananchi kutofacha watu wenye Ulemavu katika zoezi hilo kwa kisingizio cha Imani potefu.
Amesema hayo kwenye mkutano wa hadhara wa kuhamasisha Sensa katika kata ya Ulowa Wilaya ya Kahama ambapo amewaomba wananchi kusitisha shughuli zao kwa siku hiyo ikiwemo kwenda shambani na karahisisha zoezi hilo kwa makarani wa sensa.
“Kuna wengine wanawaficha watoto wenye ulemavu na kuficha taarifa zao serikali inataka kujua taarifa yao achaneni na imani potofu sisi tunataka taarifa za watu wote ili serikali iweze kuwasaidia”- Mbunge Cherehani
“Najua tupo kwenye maandalizi ya mashba kwaajili ya kilimo niwaombe ndugu zangu siku hiyo tutulie nyumbani tukishahesabiwa ndio tuendelee na shughuli zetu tusipoteze takwimu zetu kwa kisingizio cha kwenda shambani” Emmanuel Chereheni mbunge wa Ushetu