Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mh.Martin Shigella amewataka wawekezaji na wafanyabishara kutumia fursa iliyopo katika kuendelea kuwekeza ndani ya mkoa wa Geita kwani halmashauri zote zilizopo ndani ya Mkoa huo zina maeneo ya kutosha akitolea mfano Halmashauri ya Mji wa Geita kwa kutenga maeneo mengi ya uwekezaji .
Akizungumza Mara baada ya kufungua Duka la Vifaa vya Ujenzi vya kisasa eneo la Mwatulole linalofahamika kwa Dar ceramica centre Mh.Shigella amesema uwepo wa Duka hilo litasaidia kuondoa changamoto kwa wananchi wenye uhitaji wa Vifaa vya kisasa vya ujenzi waliokuwa wakiagiza nje nchi na Mikoa Jirani huku akiomba kutoa punguzo kwa kipindi hiki cha kuelekea zoezi la sensa.
Mh. Shigella ametaka wananchi wa Mkoa wa Geita kununua Bidhaa zinazozalishwa na kutengenezwa ndani ya mkoa wa geita lengo likiwa ni kukuza soko la ndani bila kutegemea vitu pamoja na Bidhaa kutoka Nje ya nchi kwani hata Rais Samia amekuwa akisisitiza kupenda vitu vyetu kama ishara ya kukuza uchumi wetu.
“Tuna uwekezaji Mkubwa unaendelea Tuna viwanda vinakuja vikubwa vya samaki lakini pia kwenye lifainali ya Gold katika Mkoa wetu wa Geita yote haya ni mazingira mazuri ya uwekezaji katika shughuli za kibiashara lakini pia mkoa wa Geita ina mbinu za utalii inayo maeneo mazuri ya utafiti yanahitaji kuendelezwa lakini pia kuweka mifumo ambayo itavutia wawekezaji, ” RC Shigella.
” Na mimi niungane na ndugu yangu waja kwa kuwaomba na kuwasihi wenzetu kuona uwezekano wa kupunguza Bei hata kwa wiki moja ndugu waja ametukumbusha sensa ambayo ni Agosti 23 ni siku ya Jumanne sasa mimi niwaombe Dar ceramica centre angalau kuanzia leo Agosti 20 mpaka Jumamosi ya wiki ijayo ya tarehe 27 ikawe kipindi cha Punguzo la Bei, ” RC.Shigella.
Kwa upande wake Meneja Mkuu wa kitengo cha Mauzo na masoko Dar ceramica Centre Tanzania Ndg.Osmas Patrick amesema wao ni moja ya wasambazaji wakubwa wa vifaa vya ujenzi vya kisasa hapa nchni kutoka Spain huku akiwataka wananchi wa Mkoa wa Geita kuchangamkia fursa hiyo ya uuzwaji wa Vifaa hivyo.
Aidha Meneja Patrick ametoa punguzo la asilimia Sita ya vifaa vinavyouzwa katika Duka hilo kwa kipindi cha wiki moja kuanzia sasa lengo likiwa ni kuwapa wafanyabishara fursa ya kuja na kuona vifaa vyao.
” Mh.Mkuu wa Mkoa na tunasema Mkuu akiomba hilo sio ombi tena ni utekelezaji naomba nikuahidi tuu Mkuu wa mkoa kwamba ombi lako tumelikubari na kuanzia leo mpaka Jumamosi inayokuja siku saba kila mteja ambaye ataingia dukani kwetu tutampunguzia kwa asilimia sita kwa chochote ambacho atanunua ukinunua kifaa cha kuwekea sabuni ukinunua Jakuzi ukinunua tailizi ukinunua mabomba kwa maana mixer utapunguziwa, ” Meneja Masoko Tanzania Patrick.
Nao Baadhi ya wadau wameipongeza kampuni ya hiyo kwa kuwapa kipaumbele wanageita na kuondoa changamoto ambazo walikuwa wakikumbana nazo za kuagiza vifaa nje ya nchi huku wakisema mkombozi sasa amewafikia wanageita.