Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Nickson Simon a.k.a Nikki wa Pili amefanya mazungumzo Mkurugenzi wa Kanda ya Kijiografia wa Shirika la Direct Aid Mr. Tariq Fahim toka Makao Makuu ya Shirika hilo yaliyopo Kuwait.
Kwenye mazungumzo yao Nikk wa Pili amemueleza Mkurugenzi huyo juu ya kampeni yake ya Kisarawe yenye ujuzi ambapo baada ya mazungumzo hayo Mr. Tariq Fahim amesema wamepanga kujenga Chuo kikubwa cha Ufundi Tarafa ya Chole ili kusaidia ajenda ya Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Nikk ya Kisarawe yenye ujuzi.
Baada ya mazungumzo hayo, Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Nickson Simon Nikk wa Pili amepokea msaada wa mitambo ya Solar 200 kwa ajili ya wananchi wa Kitongoji cha Mlegele.
Mbali na kugawa solar hizo Mkurugenzi huyo pia amezindua Mashine ya kusaga kata ya Manerumango, ameshuhudia pia ujenzi wa kisima kirefu cha shule ya Sekondari Gongoni, Ghala la Chakula Manerumango na Miradi ya Ufugaji.
Mkurugenzi huyo aliambatana na Mr Mukhtaar Sayyid Mkurugenzi wa kanda kusini mwa Afrika, Mkurugenzi Mkuu Tanzania Dr. Adam Osman na Makamu Mkurugenzi Mkuu Tanzania Mr. Mohamed Orabi.