Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi 2022, Anne Makinda akiwa Dar es salaam leo amesema zoezi la kuhesabu Watu lililoanza usiku wa kuamkia tarehe 23
Agosti 2022 hadi kufikia tarehe 29 Agosti, 2022 linaendelea vizuri ambapo kiwango cha kaya ambazo zimehesabiwa kimefikia asilimia 93.45.
•Makinda amesema”Haya ni mafanikio makubwa yaliyotokana na utayari mkubwa wa Wananchu kushiriki kuhesabiwa kwa ajili ya maendeleo ya Nchi, kulingana na ratiba ya zoezi la kuhesabu Watu ambalo linatakiwa kuhitimishwa tarehe 29 Agosti, 2022 lilitakiwa lifanyike kwa siku 7 kuanzia tarehe 23 hadi 29 Agosti, 2022″
“Aidha, taarifa zilizokwishakusanywa zinaonesha kuwa bado kuna asilimia 6.55 ya kaya ambazo hazijahesabiwa, inawezekana tusiweze kufikia kaya zote zilizobaki kwa leo na lengo letu ni kuhakikisha kila mtu anahesabiwa”
“Kutokana na hali hiyo, napenda kutoa wito kwa Wananchi wote ambao hawajahesabiwa wahakikishe wanatoa ushirikiano wa kutosha kwa Makarani wa Sensa waliopo katika maeneo yao ili wahesabiwe kabla ya leo jioni ya tarehe 29 Agosti, 2022 jioni”
“Makarani wa Sensa wapo wa kutoka katika maeneo ambayo bado kaya nyingi hazijahesabiwa, Waratibu wa Sensa katika Wilaya wamefanya utaratibu wa kuongeza Makarani kutoka maeneo ya jirani ambapo wamekamilisha kuhesabu kwenda kwenye maeneo yenye uhitaji ili kazi hiyo ikamilike kwa wakati”