Jeshi la ulinzi la wananchi Tanzania JWTZ kupitia shule yake ya Mafunzo ya awali ya Kijeshi RTS Kihangaiko,limeanza kutekeleza maelekezo ya Mkuu wa majeshi Jenerali Jocob John Mkunda,ya kuhakikisha jeshi hilo linakuwa na mahusiano mazuri na jamii inayo lizunguka jeshi hilo,shabaha ikiwa ni kurahisisha utekelezaji wa jukumu lake la ulinzi wa Nchi,raia Pamoja na Mali zao hii ikiwa ni pamoja na wakati wa vita.