Mkuu wa Mkoa wa Manyara Makongoro Nyerere ameiagiza Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) kuendeleza matumizi ya Teknolojia katika udhibiti wa huduma za usafiri ardhini ikiwa ni pamoja na matumizi ya mfumo wa Tiketi Mtandao ili kuongeza tija kwa wasafirishaji, abiria na Serikali kwa ujumla.
Ameyasema hayo katika kikao chake na Mkurugenzi Mkuu wa LATRA CPA Habibu J. Suluo kilichofanyika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara mjini Babati, kilichohudhuriwa na Katibu Tawala Mkoa wa Manyara Bi. Caroline Mthapula na baadhi ya maafisa wa LATRA ikiwa nisehemu ya ziara ya Mkurugenzi Mkuu wa LATRA mkoani humo.
‘Nilipata bahati ya kujifunza zaidi kuhusu mfumo huuambao nilikuwa nikiusikia, baada ya kukaa nawataalamu nimegundua kuwa mfumo wa Tiketi Mtandao unamsaidia mmiliki wa basi kukusanyamapato yake kwa ufanisi zaidi, unamrahisishia abiriakununua tiketi kwa urahisi na unaisaidia Serikali kukusanya mapato kwa ufanisi’ alisema.
Aliongeza kuwa, mfumo huo unasaidia kudhibiti upandishaji holela wa nauli kipindi cha mahitaji makubwa ya huduma ikiwemo kipindi cha sikukuu zamwisho wa mwaka.
Aidha, Nyerere emeiagiza LATRA kuongeza utoaji wa elimu na kuwafikia wadau wengizaidi kwa kuwa matumizi ya teknolojia ndiyo muafaka wa kuleta mapinduzi katika sekta ya usafirinchini.
‘Tunakoelekea ni abiria kuweza kujihudumia mwenyewe bila kutegemea kuhudumiwa na mtu, labda mizigo ndiyo itahitaji kuhudumiwa, kwa kuwa Tanzania ni sehemu ya dunia, maendeleo hayo hatuwezi kuyaepuka’
Amesema kuwa ofisi yake itaendelea kushirikiana na LATRA ambapo ameiagiza LATRA kuendeleza ushirikiano na wadau wote wakiwemo Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani na wasafirishaji ili kuongeza tija katika sekta ya usafirishaji ambayo inatoa ajira nyingi kwa wananchi na kusaidia kufikia malengo ya Serikali ya awamu ya sita inayoongozwana Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kwa upande wake, CPA Suluo ameahidi kufanyia kazi maelekezo ya Mkuu huyo wa Mkoa na kuendeleza ushirikiano na elimu kwa wadau wote ilikuwezesha Serikali kufikia malengo yake kwa wakati.
Katika ziara yake Mkoani Manyara, CPA Suluo alipata fursa ya kutembelea wadau mbalimbali wakiwemo Kamanda wa Polisi Mkoa wa ManyaraACP George Katabazi na Kaimu Mkuu wa Usalama Barabarani Mkoa wa Manyara ASP Mahenda Keraambapo walipata fursa ya kujadili masualambalimbali ya ushirikiano ikiwemo utekelezaji wamatumizi ya mfumo wa Tiketi Mtandao.
Mhe. Makongoro Nyerere akiwa na CPA Suluo katikaofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara, wa kwanza kushoto ni Katibu Tawala Mkoa wa Manyara Bi. Caroline Mthapula na wa kwanza kulia ni AfisaHabari – LATRA Bw. Salum Pazzy.
Mhe. Makongoro Nyerere (wa kushoto) katika pichaya pamoja na CPA Suluo katika ofisi ya Mkuu waMkoa wa Manyara
CPA Suluo (wa kushoto) akiwa ofisini kwa Kamandawa Polisi Mkoa wa Manyara ACP George Katabazi, wa kwanza kulia ni Afisa Mfawidhi LATRA Mkoa waManyara Bw. Joseph Michael