Mkoa wa Morogoro kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo ya kilimo wakiwemo baraza la kilimo nchini umeandaa kongamano la maonesho ya kilimo yajulikanayo kama kilimo marathon lenye lengo la kuhamasisha jamii kushiriki katika shughuli za kilimo kama sehemu muhimu ya kuchangia pato la taifa.
Akizungumza katika kikao cha wadau wa kilimo Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Fatma Mwasa amesema maonesho hayo yanataanza spetemba 29 hadi Octoba Mosi mwaka huu katika Uwanja wa Jamhuri Manispaa ya Morogoro huku akiwataka wadau kushiriki kikamilifu ili kuhakikisha jamii inapata elimu zaidi ya kilimo.
Mwasa amesema nia ya Serikali ni kuhakikisha Sekta kilimo inaendelea kuwa Sekta muhimu kwa Uchumi wa nchi na mtu moja moja hasa vijana ambao wamekuwa wakisahaulika katika masuala ya kijamii.
Katika maonesho hayo Wananchi watapata fursa ya kupata Elimu ya kilimo Bora ,masoko na suala la utunzaji Mazingira ambapo kilimo kimekua moja ya sababu za uharibifu wa mazingira kwa kulima katika vyanzo vya maji,misitu ya hifadhi hivyo maeneosho hayo yatatoa elimu ya utunzaji mazingira.
Naye Katibu tawala msaidizi uoande uchumi mkoa Morogo Dkt. Rozaria Rwegasira anasema uwepo wa kongamano hilo utasaidia wakulima wengi hasa vijijini kupata elimu ya Kilimo bora.