Wakati Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mh.Fatma Almas Nyangasa akizungumza alipotembelea na kufanya ukaguzi Mradi ujenzi wa bweni la wasichana wenye mahitaji maalum lililopo Chekeni Mwasonga shule ya Msingi.
Akizungumza katika ziara hiyo amesema ni matarajio kuwa kuanzia January mwakani shule hiyo ambayo inakuwa shule ya ya kwanza ya watoto wenye mahitaji maalum itaanza ambapo kwa Kigamboni hakukuwa na shule ya wenye mahitaji hivyo ni Mradi mkubwa na wa kujivunia sambamba na hilo yataongezwa madarasa mengine mawili na mengine manne yatafanyiwa ukarabati tayari kwa ajili ya kuanza kutumika hiyo January Mradi huo umekamilika kwa 95% na utagharimu shilingi mil.127 ambazo mil.80 ni pesa za uvico 19 na mil.47 na 24 elfu ni fedha za mapato ya ndani ya Manispaa ya Kigamboni.
Aidha amesema kwa bajeti hii ya 2022/2023 kiasi cha bil 1.937 zimetengwa kwa ajili ya miradi elimu mipya na ukarabati wa miradi ya shule za Msingi kwa Wilaya ya Kigamboni,kutokana na hilo amemshukuru Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Samia Suluhu Hassan kwa kuwezeaha Kigamboni kupata fedha hizo kwa ajili ya Miradi ya elimu.