Rais Samia leo amekata utepe kuzindua magari 50 kati ya 200 ya Maafisa Elimu Sekondari nchini na pikipiki 50 kati ya 517 za Maafisa Lishe kwa ajili ya kuimarisha utoaji wa Huduma za Afya Msingi na Elimu Sekondari kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini.
Rais Samia amezindua magari hayo leo wakati akishiriki hafla ya utiaji saini Mkataba wa Usimamizi wa Shughuli za
Lishe na tathmini ya sita (6) ya Mkataba wa Lishe uliofanyika Ukumbi wa Jiji la Dodoma – Mtumba, leo tarehe
30 Septemba 2022.
“Vifaa vote vina thamani ya Tsh. Bil 94.4, nilikuwa nanong’ona na Waziri wa Afya, nikawa namwambia tupige break kidogo kwenye
ujengaji wa vituo hasa kwenye kata, tujielekeze zaidi kwenye kumalizia Zahanati lakini tujielekeze sanaa kwenye kuimarisha huduma kwenye vituo vya kata kwa kuhakikisha vifaa tiba na vingine vinapatikana na Watumishi wanakuwepo katika maeneo hayo ikiwa ni pamoja na nyumba za Watumishi, nahisi haya yatasaidia kuliko kuendelea kujenga kujenga”
“Watakaopata vifaa hivi twende tukasimamie matunzo, sitovumilia kusikia miezi sita mwaka mmoja kifaa hakina kazi kimekaa pembeni, aliyeagiza atanieleza a Mtumiaji atanieleza”