Rais Samia amewaapisha Mawaziri wapya watatu aliowateua jana ambao ni Waziri wa ulinzi Innocent Bashungwa, Waziri wa TAMISEMI Angellah Kairuki na Waziri wa mambo ya nje Dr. Stergomena Tax ambapo baada ya kuwaapisha ameongea yafuatayo.
“Mh Angellah Kairuki si Mgeni kwenye kazi hii ulishafanya sana na kipindi ambacho ulikuwa nje umejifunza mengi na nimeona sasa tayari urudi unisaidie, TAMISEMI ni ileile uliyoiacha kuna mambo mambo tutaitana tuelekezane nini cha kufanya huko ndani”- Rais Samia
“Katika viapo vyetu tunaapa kuilinda na kuitetea Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ni dhana yangu kwamba Waheshimiwa kile kiapo kinakuwa cha kweli lakini pia la pili kujua mipaka kwamba Nchi hii ina Mamlaka na Mamlaka uliyowekewa ina mipaka yake na ukitaka kuivuka lazima upate ruhusa ya Mamlaka ya juu”- Rais Samia
“La tatu ni siri unapotaka kuisema ujue jinsi ya kuitumia kufanya kazi, linaloamuliwa na Serikali wewe kama Waziri ni lako, huwezi kusema nimeelekezwa hivi Mimi sikutaka hivi lakini imebidi nifanye hivi kwasababu nimeelekezwa, huwezi kujitoa, nilitaka kuwaambia hayo”- Rais Samia.