Mwanafunzi wa darasa la saba katika shule ya msingi Shahende kata ya Butobela wilayani Geita, Helena Mashaka (13) ameshindwa kufanya mitihani ya kuhitimu elimu ya msingi baada ya kuchomwa moto na mama yake mzazi.
Mitihani ya taifa kwa watahiniwa wa elimu ya msingi inafanyika nchi nzima kwa siku mbili, Oktoba 5 na 6.
Mtendaji wa kijiji hicho Edar Michael amesema alijulishwa kuhusu tukio hilo na mwalimu mkuu wa shule ya Shahende kuwa Helena ameshindwa kufanya mtihani wa taifa kwakuwa mikono yake imechomwa moto na mama yake mzazi.
Baada ya kukamatwa na kuhojiwa, Mama wa Helena huyo alidai kuwa alimchoma moto binti yake baada ya kubaini alimuibia shilingi elfu thelathini.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti huyo, Mama wa Helena anashikiliwa katika kituo cha Polisi kata ya Bukoli na tayari itoto huyo amepatiwa matibabu katika zahanati ya Bukoli na anaishi nyumbani kwa Mwenyekiti huyo huku taratibu zaidi zikiendelea kufuatiliwa ili afanye mtihani mwaka 2023.
MASANJA KAJIBU KALI YA MWAKA “HATA NIMKUTE MKE WANGU ANAPIGA GAME SIMUACHI”