Jamii imetakiwa kuwajibika zaidi katika maswala mbalimbali ya kifamilia pamoja na kutokufungia macho vitendo via ukatili wa kijinsia vinavyosababisha kuvunjika kwa ndoa pamoja na migogoro mbalimbali inayotokea kwenye familia nyingi hapa nchini.
Wito huo umetolewa na Waziri wa maendeleo ,jamii,jinsia wanawake na makundi maalum,mheshimiwa Dr.Doroothy Gwajima, wakati akifungua Kongamano kubwa la wanandoa na familiaa katika mkoa wa Dar es Salaam lililofanyika siku mbiii lilioandaliwa na Shirika lisilo la kiserikali la Tanzania Marriage and Child care Foundaation TAMCARE kwa kushirikiana na serikali pamoja na taasisi ya ustawi wa jamii.
Amesema imefikia wakati sasa wakuwepo kwa sheria ambayo itaibana mmoja kwa mmoja jamii husika juu ya matukio ambayo yamekuwa yakitokea katika familia nyingi ikiwemo kuvunjika kwa ndoa pamoja na kuwepo kwa migogoro mingi ya kifamilia,kwasababu jamii ndio inayoshuudia matatizo hayo kwa kiasi kikubwa kuanzia yanapoanzia hadi yanapofikia hatua kubwa zaidi.
Aidha amewataka wadau na mashirika yasioyakiserikali yanayoshughulikia maswala ya ndoa na familia ikiwemo taasisi ya ustawi wa jamii kufwatilia na kuangalia mfumo uliopo katika baadhi ya vyombo vilivyoundwa na serikiali vyenye dhamana katika maswala hayo,iwapo mfumo wake ni rafiki na unafikika kirahisi kwanzia ngazi za chini kabisa ili kuona namna ambavyo mfumo huo unaweza kuwa na nguvu ya kutosha katika kudhibiti migogoro na kuvunjika kwa ndoa mapema inapoanza kabla ya tatizo kukomaa na kushindwa kupata ufumbuzi.