Spika wa zamani wa Bunge, Job Ndugai amesema kumekuwa na maoni tofauti kwamba Wabunge wapelekwe Mirembe na kupimwa afya ya akili kwanza kabla ya kwenda kuomba ridhaa ya kuwawakilisha Wananchi na kusema jambo hilo ni la kuwaachia Wananchi ili waone kama lina umuhimu ama laah.
Ndugai ametoa kauli hiyo October 10, 2022 katika Hospitali ya Mirembe kwenye Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Afya ya Akili Duniani.
“Hata kule Bungeni kuna wakati huwa panatolewa wito kwamba Wabunge wapimwe akili, wapelekwe Mirembe kwanza kabla ya kupata Clearence, tunapojaza fomu zile za kuomba ubunge tujaze fomu kisha tuje Mirembe tupimwe na katikati ya muhula tupimwe tena, hili maana yake ni pamoja na Madiwani na Viongozi wengine wakuchaguliwa, sijui kama jambo hilo ni muhimu ama si muhimu lakini kuna wengine wanasisitizaga kwelikweli jambo hilo, lakini hilo ni la Wananchi niwaachie Wananchi”