Club ya Yanga leo imetangaza kuingia mkataba na Shirika la Umoja wa Mataifa la UNICEF kwa ajili ya kusaidia jamii katika utoaji wa elimu ya kujikinga na UVIKO-19 na Ebola.
Taarifa za mkataba huo zimetangazwa leo na Rais wa Yanga SC Hersi Said mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
“Leo kwa mara ya kwanza katika historia tumeingia Mkataba na Taasisi kubwa ya umoja wa mataifa (UNICEF). lengo kubwa la mkataba huo ni kutoa elimu ya kujikinga virusi vya Uviko-19 na Ebola”>>> Hersi Said
“Ni heshima kubwa kuingia mkataba na umoja wa mataifa ni kwa mara ya kwanza katika historia kwa vilabu vya hapa Afrika Mashariki, pia ushirikiano na UNICEF umejengwa katika falsafa ya Klabu ya kusaidia jamii”>>> Hersi Said