Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA), mkoani Geita imewaomba wafanyabiashara wilayani Nyang’hwale kusajili na kurasimisha biashara zao kwa kupata TIN-Namba ili kukidhi vigezo vya kupata tenda mbalimbali.
Ofisa Elimu na Huduma kwa Mlipa kodi Mkoa wa Geita, Justine Katiti amebainisha hayo wakati akizungumuza na wafanyabiashara wa eneo la Busolwa na Kharumwa wilayani humo.
Aidha Katiti amewaeleza wafanyabiashara wanapaswa kujenga utamaduni wa kuweka kumbukumbu ya biashara kwani kutofanya hivyo kunawanyima fursa ya kukopesheka kwenye taasisi za kifedha kwa kukosa taarifa sahihi.
Amesema ili kupata kumbukumbu sahihi za biashara ni vyema watumie Mashine za Kielektroniki (EFD) na kuepuka kufanya makadirio yasiyo sahihi na yenye udanganyifu.
“Kutoa risiti kila bidhaa inayouzwa ni takwa kisheria tunaendelea kuwakumbusha ukiuza toa risiit na mteja ukinunua dai risiti,”- Ndg Katiti.
Ameongeza “Tunafahamu changamoto za biashara ukiona umepata changamoto tupe taarifa kwa maandishi ili kuondokana na faini zisizo na tija.”
Mmoja ya Wanyabiashara waliopatiwa elimu Nyang’hwale, ni Ndg Julius Clement amesema TRA itaendelea kuwa karibu na wafanyabiashara na kuwakumbusha kila mmoja wajibu wake.
Amesema Mikutano ya uelimishaji inasaidia TRA kufahamu changamoto mbalimbali za walipa kodi na kuondoa vikwazo visivyo na tija kwenye biashara.