Watu wanne wamenusurika kifo katika ajali iliyohusisha magari mawili ya mzigo moja aina ya fuso lenye namba za usajili T 496 DDB lilikua linatokea Dar kwenda Morogoro Mjini kugongana uso kwa uso na Lori lenye namba za usajili T 248 EAE lilikua linatokea Songea kuelekea Dar .
Kamanda wa Polisi Mkoa Morogoro Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa polisi ( SACP) Fortunatus Musilimu amesema ajali hiyo imetokea asubuh ya leo octoba 20 mwaka huu 2022 katika eneo la Nanenane Manispaa ya Morogoro.