Mbunge wa Jimbo la Msalala ,Halmashauri ya Msalala Mkoani Shinyanga Ndg.Kassim Idd amewagawia Viongozi wa Mitaa mbalimbali wakiwemo Mabarozi pamoja na wenyeviti wa vitongoji na vijiji Majembe kwa ajili ya kilimo huku akiwahasa kutumia vyema Msimu huu wa kilimo cha Dengu.
Akizungumza Mara baada ya kukutana na wananchi wa Jimbo lake ambapo Viongozi mbalimbali wa Mkoa wamehudhuria kikao hicho akiwemo Katibu tawala wa Mkoa huo pamoja na Kaimu Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Usimamizi wa stakabadhi za Ghala Mbunge Kassim amewataka wananchi kuendelea kushirikiana katika kukuza zao la dengu katika Jimbo hilo.
“Baada ya Mheshimiwa Rais kutupatia fedha Milioni mia Moja na Hamsini kwa ajili ya ruzuku ya Mbolea lakini pia kutupatia mbegu za pamba bure na madawa Bure na mimi kama mbunge nimeona sasa kumuunga Mkono mabarozi wetu hawa walioko hapa Mwenyekiti wa chama yuko hapa atawagawia jembe moja moja kila barozi ataondoka na jembe moja moja ili aende akaonyeshe kwamba anafanya kazi kwa bidii, ” Mbunge Kassim.
Mbunge Kassim amezungumzia suala la Baadhi ya wakandarasi ambao wamekua wakishindwa kukamilisha miradi mbalimbali ikiwemo miradi ya Mabarabara na kusema wakandarasi hao wataendelea kupambana nao lengo likiwa ni kuijenga Msalala.