Binti anayefahamika kwa Jina la Janeth Charles miaka 18 Mkazi wa Mtaa wa Nyakahangola na Mwanafunzi wa kidato cha tatu katika shule ya Sekondari Nyabubele iliyopo kata ya kasamwa Mkoani Geita amefariki Dunia kwa kunywa sumu ya panya.
Akizungumza na ayo tv Baba wa Marehemu aitwaye Charles Lugwesa amesema tukio hilo lilitokea Majira ya Saa kumi na Moja jioni kuwa Binti yao alidai kusumbuliwa na tumbo hali ambayo iliwapelekea wazazi wote wawili kumchukua na kumpeleka zahanati ambako alipewa matibabu kwa mda mfupi na kisha kukata roho.
“Nilimtafutia huduma ya kwanza hapo kwenye Zahanati nilipompeleka Zahanati akapokelewa wakaanza kushughulika nae Madaktari lakini hatukufanikiwa lolote mtoto akazidi kuwa na hali mbaya mpaka kufariki Dunia Mda wa saa nane uchunguzi wa Madaktari maana hapa kipimo hakipo cha sawa sawa yeye mwenyewe ambaye aliyekuwa Mgonjwa kipindi cha kuzidiwa kabisa akiwa mwishoni mwishoni sasa alisema nimekunywa sumu, ” Baba Mzazi wa Marehemu.