Katibu Tawala mkoa Morogoro Dokta Mussa Ally Mussa amemtaka Mkurugenzi Manispaa ya Morogoro kuongeza nguvu katika ukusanyaji Mapato kwa kipindi cha robo tatu mwaka kilichobaki.
Dk Mussa ameyasema hayo wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani Halmashuri Manispaa ya Morogoro ambapo amesema kwa kipindi cha robo mwaka kuanzia mwezi julai Hadi September halmshauri hiyo imekusanya asilimia 24 tu ya mapato na kushika nafasi ya mwisho kati ya halmashauri tisa za mkoa Morogoro na kutakiwa kuongeza nguvu katika ukusanyaji Mapato ili kufikia malengo waliyojiwekea.
Amesema Hadi Sasa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi inaongoza kwa kipindi hiki Cha robo ya kwanza ya mwaka kwa kukusanya asilimi 60 huku halmashauri zingine zikikusanya chini ya hizo Jambo ambalo linaonesha kutomridhisha Katibu Tawala.
Kwa upande wake Mkurugenzi Halmashauri Manispaa ya Morogoro Ally Machela amesema kwa mwaka wa fedha 2022/2023 wamejiwekea malengo ya kukusanya Bilioni 12 tofautu na halmashauri zingine zimejiwekea malengo kidogo jambo linalosababisha kuonekana ya mwisho katika ukusanyaji mpato huku hadi Sasa wamekusanya zaidi ya asilimia 24.
Machela amesema Hadi ikifika robo tatu tayari watakua wamekusanya kiasi kikubwa Cha fedha kutokana na miradi mbalimbali waliyoiweka ikiwemo mradi wa kuuza viwanja utakao ingiza zaidi ya bilioni 2
Naye mstahiki Meya Manispaa ya Morogoro Pascal Kihanga ametoa wito kwa madiwani Kushirikiana na watendaji wa mitaa na kata katika ukusanyaji Mapato