Wabunge wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo November 5, 2022 wakati wakichangia mjadala kuhusu taarifa za kamati tatu za bunge kuhusu taarifa ya mdhibiti na mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka wa fedha ulioshia June 30 2021, wameonesha kutopendezwa na ubadhirifu wa mali za umma ambao umebainishwa kwenye ripoti ya CAG na kuliomba bunge kuazimia kuchukua hatua kwa watendaji wote waliobainika kuhusika na ubadhirifu wa mali za umma.
Miongoni mwa wabunge waliochangia ni mbunge wa Viti Maalum Kunti Majala.