Wabunge wamechangia mjadala kuhusu taarifa za kamati tatu za bunge kuhusu taarifa ya mdhibiti na mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka wa fedha ulioshia June 30 2021 na wameonesha kutopendezwa na ubadhirifu wa mali za umma ambao umebainishwa kwenye ripoti hiyo.
Mbunge wa Makete Festo Sanga ni miongoni mwa waliosisimama leo November 5 2022 na kusema kuwa kabla ya kuchukua hatua zingine kwa wabadhirifu waliobainishwa kwenye ripoti ya CAG waorodheshwe na iitwe “List of shame” yaani orodha ya aibu Serikalini kwa mawakala, taasisi na halmashauri nchini.
Baadhi ya jambo Mbunge Sanga anatamani liorodheshwe kama “List of Shame” ni pamoja na Mamlaka ya Maji na usafi wa mazingira Dar es salaam kudaiwa kukusanya zaidi ya MILIONI 755 kwa kukadiria bili za maji.
“Hawa watu wasione kama sisi tunapiga story ni muda muafaka wa kiti chako Mheshimiwa Spika kuonyesha kwamba tuna msuli wa kulipigania Taifa letu na uwezo wa kuwaadabisha”