Ndege ya Precision Air iliyopata ajali Bukoba, Kagera juzi na kusababisha vifo vya Watu 19 imetolewa kwenye maji hii leo huku timu ya Wataalamu ikiendelea na uchunguzi.
Mamlaka ya Anga nchini imetangaza kuwa uwanja wa ndege wa Bukoba utafunguliwa ili kuendelea na operesheni za ndege kama ilivyokuwa awali huku Ndege ya Air Tanzania ikitarajiwa kutua kesho.