Cristiano Ronaldo katika mahojiano yake maalum na mwanahabari Piers Morgan ambayo wengi wanaamini ndio safari yake ya kuondoka Man United amekosoa vikali maamuzi ya viongozi wa Man United.
Ronaldo amekosoa kitendo cha Viongozi kumfuta kazi Kocha Ole Gunnar Solskjaer na kumuajiri Ralf Rangnick ambaye alikuwa hayupo kwenye kazi ya ukocha na amekuwa akisifika kama Mkurugenzi wa michezo na sio Kocha.
“Kwa mfano inawezekanaje club kama Man United inamfukuza kazi Ole (Gunnar Solskjaer) na kumleta Mkurugenzi wa michezo Ralf (kuwa Kocha) ni kitu ambacho hakuna anayeweza kuelewa”
“Huyu mtu (Ralf) sio hata Kocha, club kubwa kama Man United inamleta Mkurugenzi wa michezo (Kuwa Kocha Mkuu wa timu) hili suala halikunishangaza mimi bali dunia nzima”